Navigation
 Portal
 Index
 Memberlist
 Profile
 FAQ
 Search
October 2019
MonTueWedThuFriSatSun
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031   

Calendar Calendar

Statistics
We have 980 registered users
The newest registered user is jaimish

Our users have posted a total of 1236 messages in 349 subjects
Who is online?
In total there are 4 users online :: 0 Registered, 0 Hidden and 4 Guests

None

[ View the whole list ]


Most users ever online was 74 on Wed May 15, 2019 7:44 pm

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Re: Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  ALLY MUNIR on Sat Apr 27, 2019 6:05 pm

GWK wrote:UWEZO
Nashukuru kwa kumsaidia mdau wa jukwaa anayejulikana kama mhandisi.

Naomba vilevile kupata mtazamo wako kuhusu swali la RJM kwamba kama document zinauzwa na akarudisha mzabuni ambaye hajanunua zabuni yake ifanyweje. Inawezekana kuipata kwa mtandao, kunakilisha kabrasha halisi au hata kupewa na watumishi wasio waaminifu.

Naomba mchango kwa hili pia.

Ndugu, zabuni zote ambazo zinauzwa/zinazotolewa kwenda kwa wazabuni ni lazima kurekodiwa ili iwe ni kumbukumbu wakati wa ufunguzi kuweza kujuwa ni wazabuni wangapi wamenunua/wamepewa zabuni. sasa ikiwa kuna mzabuni amewasilisha zabuni wakati hakuwepo kwenye list ya zabuni zilizouzwa/zilizotolewa zabuni yake haitapokelewa kwa sababu haikufuata vigezo husika. hivyo wazabuni wanatakiwa wawe makini wakati wakipewa zabuni kuhakikisha kwamba zabuni zao zimerekodiwa na kusaini kwenye list ya zabuni zilizouzwa.

ALLY MUNIR

Posts : 3
Join date : 2013-04-02
Location : Dar es Salaam

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Re: Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  GWK on Fri Apr 17, 2015 2:05 pm

UWEZO
Nashukuru kwa kumsaidia mdau wa jukwaa anayejulikana kama mhandisi.

Naomba vilevile kupata mtazamo wako kuhusu swali la RJM kwamba kama document zinauzwa na akarudisha mzabuni ambaye hajanunua zabuni yake ifanyweje. Inawezekana kuipata kwa mtandao, kunakilisha kabrasha halisi au hata kupewa na watumishi wasio waaminifu.

Naomba mchango kwa hili pia.

GWK

Posts : 55
Join date : 2014-03-24
Age : 52
Location : DAR ES SALAAM

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Kukosekana risti ya ununuzi wa tenda

Post  uwezo on Thu Apr 16, 2015 12:40 am

GWK kwanza pole sana,
Naomba kujikita kwenye suruhisho la tatizo, Taasisi nunuzi inatakiwa kutumia procurement procedural form issued by PPRA. F.8 & 9 zinaonyesha kumbukumbu za zabuni zilizowasilishwa na zilizofunguliwa na kumbukumbu hizi wanapaswa kupewa timu ya tathmini ya zabuni ili kusaidia katika kutathmini zabuni. Kanununi Na 204 na 205 za ununuzi katika sekta ya umma zinaainisha makosa ambayo zabuni inaweza kudhibitika na makosa ya kisheria na kukataliwa. Hata hivyo, kutoweka risiti za kununulia nyaraka ya zabuni si miongoni mwa makosa hayo.

uwezo

Posts : 15
Join date : 2012-07-24

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Re: Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  GWK on Tue Apr 07, 2015 5:00 pm

RJM
Namefurahi kwa swali lako ambalo sijawahi kujiuliza japo inaweza kutokea mzabuni akapata documents bila kuzinunua. Mzabuni aliyepata docs kwa njia nyingine (bila kuzinunua sehemu husika ambapo atapewa risiti) haruhusiwi kushiriki. Manunuzi ni mchakato uliowekewa taratibu za kufuatwa hadi mwisho. Aliyepata docs kwa njia nyingine hatashinda zabuni husika (amekiuka utaratibu wa manunuzi)

Aidha, mjadala wa awali ulikuwa kwamba mzabuni amenunua zabuni lakini hakuambatisha risiti kwenye kabrasha hivyo wakati wa ufunguzi haikuonekana na hivyo zabuni kuzuiwa kufanyiwa tathmini. Kwa mazingira haya kamati ya tathmini ingeona hilo kuwa kosa dogo na kulishughulikia ipasavyo ikiwemo kuangalia kwenye kumbukumbu mbalimbali za taasisi nunuzi zikiwemo orodha ya wazabuni walionunua, nakala za risiti zilizouzia makabrasha ya zabuni hiyo (verification) na wakijiridhisha kwamba mzabuni alinunua kabrasha hilo tathmini inaendelea.

GWK

Posts : 55
Join date : 2014-03-24
Age : 52
Location : DAR ES SALAAM

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Re: Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  RJM on Mon Mar 30, 2015 2:08 am

GWK,

Inawezekana wakati wa kufungua quotations risiti isionyeshwe. Je? kama quotaton documents zilikuwa zinaunzwa? Je mzabuni anaweza kushiriki bila kununua document?
RJM
RJM

Posts : 258
Join date : 2009-07-30
Age : 69
Location : What is written without effort is in general read without pleasure

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Re: Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  GWK on Thu Feb 26, 2015 3:35 pm

Mhandisi:
Kwa maoni yangu suala la kutoambatisha risiti ya ununuzi wa tender document sio kosa la kufanya mzabuni aenguliwe tena wakati wa ufunguzi. Kinachoweza kufanya zabuni isifanyiwe tathmini na kamati ya kitaalam ya tathmini ni zabuni iliyochelewa. Sijawahi kusikia/kuona tathmini ikifanywa wakati wa ufunguzi. Hivyo zabuni zilifuata mkondo sahihi wa tathmini na mshindi kupatikana kwa mujibu wa maelekezo kwa wazabuni (Instruction to Tenderers). Hakuna kifungu kinachoelekeza kutoambatisha risiti zabuni isifanyiwe tathmini.

GWK

Posts : 55
Join date : 2014-03-24
Age : 52
Location : DAR ES SALAAM

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  mhandisi on Thu Feb 19, 2015 8:58 pm

Katika tenda fulani kwa njia ya Quoatation iliyotangazwa wazabuni 5 walinunua vitabu.

Wakati wa ufunguzi wa tenda hadharani ilionekana hakuna mzabuni aliyeambatanisha risiti hivyo baadhi ya wajumbe walihoji hali hiyo ambapo afisa aliyehusika alitoa ufafanuzi kuwa wazabuni husika walinunua vitabu na kuonesha rejesta yenye saini iliyotumika kuuzia zabuni hizo. Wajumbe wote wakiwemo wawakilishi wa waomba zabuni waliridhia maelezo hayo na kuzikubali quotation zote kuingia katika upembuzi.

Baada ya mchakato kukamilika na accounting officer kutoa barua intention ya ku-accept kutolewa mzabuni mmoja aliyeshindwa akaamua kutumia sababu ya kutokuwa na risiti kama ni irregularity katika zabuni na kuifanya kuwa sababu ya appeal kwa Accounting officer. Je, ipi haki yake kisheria?
Na kwa kuwa litakuwa ni kosa la Accounting officer ni zipi remedies kwa mzabuni aliyepewa barua ya intention ya award of contract (winner) iwapo Accounting officer ataamua in favor of the appealant?


Last edited by mhandisi on Thu Feb 19, 2015 9:01 pm; edited 1 time in total (Reason for editing : typing error)

mhandisi

Posts : 1
Join date : 2015-02-19

Back to top Go down

Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda Empty Re: Kukosekana risiti ya ununuzi wa tenda

Post  Sponsored content


Sponsored content


Back to top Go down

Back to top


 
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum